Mkosoaji wa mitindo ya mavazi na muigizaji wa Marekani, Joan Rivers afariki

Mkosoaji maarufu wa mitindo ya mavazi 'Fashion Police', Joan Rivers amefariki September 4 akiwa na umri wa miaka 81.

Binti yake Melissa amethibitisha kifo chake katika tamko alilolitoa kupitia US Weekly.




"Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha mama yangu, Joan Rivers. Amepumzika kwa amani majira ya saa 7 na dakika 17 mchana akiwa amezungukwa na familia na marafiki wa karibu." Ameeleza Melissa katika sehemu ya tamko lake.

Joan Rivers ambaye pia alikuwa comedian na mwandishi alizaliwa June 8,1933, Brooklyn, New York, Marekani. Na alianza kupata umaarufu miaka ya 1960 alipoanza kuonekana kwenye vipindi vingi vya TV.

Apumzike kwa amani. Amina!
Previous Post Next Post