Rapa wa Bongo Flava mwenye umri mdogo, M Rap Lion amesema kuwa, kutokana na hali halisi sasa ya vijana kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo, yeye akiwa kama mfano kwa mashabiki wake ameamua kuachana kabisa na masuala ya mapenzi.
M Rap amesema kuwa, amechukua uamuzi huu kutokana na ukweli kuwa kwa sasa hakuna mapenzi ya ukweli, na kwa nafasi kama yake, wasichana wamekuwa wakivutiwa zaidi na jina lake kuliko mapenzi ya kweli.