Johari adai hajawai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray, ila Ray ni swahiba wake

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Blandina Chagula maarufu kama Johari, ambaye ni ‘business partner’ wa msanii mwenzake, Vicent Kigosi aka Ray, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na Ray pamoja na mipango yake ya kuolewa.


Muigizaji wa Filamu Bongo Johari


 Johari alisema anashangazwa kuwaona watu wakivumisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ray.

“Mimi na Ray cha kwanza ni mtu na swahiba wake, cha pili ni kama kaka yangu kwasababu tumekaa kwa muda mrefu sana. Tumefanya kazi kama partner wangu, tuna ukaribu ambao upo kikazi zaidi na kampuni yetu, lakini uhusiano mwingine ambao watu wanauzungumzia sidhani kama upo ni maneno ya watu,” amesema. “Hatujawahi kutokea uhusiano wa kimapenzi na Ray. Unajua kuna watu wanaongea vitu vya kubuni, mimi na Ray tunafanya kazi kampuni moja na wote ni wakurugenzi kwahiyo ina maana tungekuwa tuna ugomvi tungevunja kampuni. Lakini kitu kama hicho hakipo na bado tunafanya kazi vizuri na tunaheshimiana na kila mmoja kampuni inampatia maisha mazuri. Kwa sasa sijaolewa lakini siwezi kuweka wazi sana mahusiano yangu kwa sababu muda haujafika ila muda utakapofika tutawaweka watu wazi. Nitawaweka wazi hivi mbioni kwa sababu zangu. Inaweza ikawa ni mapema zaidi ila natawataka watu wasubiri ili waone nini kitatokea,” aliongeza Johari.

Pia Johari alizungumzia jinsi ambavyo wanashare kampuni ya RJ pamoja na mipangilio ya kutoa kazi zao.

“Kazi zangu zote ninazotoa zinatoka ndani ya RJ Company lakini kwa sababu kwenye kampuni ni yetu wote na wote ni wakubwa tunapishana katika kutoa kazi,” anasema. “Pia hata wasanii ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yetu tunajaribu kupishanisha ili kuleta manufaa mazuri katika kazi tunazofanya. Kampuni ya RJ Company ni kampuni mbayo imesajiriwa ina TIN namba, yaani ni kampuni kama kampuni nyinge kubwa na sidhani kama inaweza kuvunjika kwa sababu tulikotoka na tulipo sasa hivi ni mbali sana. Kwahiyo kampuni kama kampuni inafanya kazi zake vizuri na haiwezi kuvunjika leo wala kesho kwakuwa kila mtu ananufaika vizuri na hiyo kampuni.”
Previous Post Next Post