Haya ndiyo majibu ya Nisher kwa waliomkosoa juu ya video mpya aliyoifanya

Jumapili iliyopita director Nisher aliachia video mpya ya msanii aitwaye AMA G kutoka Mwanza, ikiwa ni video ya sita kutoa toka mwaka huu umeanza.



Baadhi ya mashabiki wa kazi zake wamepongeza kwa kuendelea kufanya video nzuri, lakini baadhi yao wameonekana kutoridhishwa na kiwango cha msanii aliyemfanyia video hiyo.


Nisher aliwajibu hivi kwa wale waliomkosoa kuhusu msanii aliyemfanyia video:


"Ok Seriously this has to Stop! Kwanza Ieleweke kabisa Kua saivi mimi nipo Very Expensive Kufanya Videos TZ... Nakama Hamja Shtukia nimepunguza kasi yakutoa Kazi Mpya, Kwanini? Watu Hawataki kutoa hela!!! Hiyo sio changamoto kwangu, ni changamoto ya Wasanii... Kitendo cha Huyu Kijana Ku-WEZA kunilipa kufanya Music Video Yake shilingi MILIONI 5 CASH na Kuja Onset na Pamba zake tu, Kwahilo NAMSIFU SANA!!! Bado aliniambia alitumia milioni moja zaidi kwaajili ya Kusafiri kutoka Mwanza Kuja Arusha, na kulipia hotel yake pamoja na Kuandaa mavazi Nilio Mtajia pamoja na Kulipa extra cost Zote! Namsifu sana... Pili ieleweke kua Huyu bado ni Msanii mchanga, Alichoniomba Nikwamba Nimasaidie tu Kupata Jina Langu (NISHER) kwenye kazi yake... Na aliniambia kabisa Kwamba anajua yeye bado mchanga ila aliniomba Sana kwa moyo wote akasema Yupotayari Kunilipia Gharama zozote zile ili tu Apate Jina Langu kwenye Kazi yake!!! Huyukijana Anatakiwa Apigiwe makofi... Tena amewaaibisha watu wote wenye nyimbo nzuri walioshindwa kunilipa... You should be ASHAMED OF YOURSELVES KWA KUMPONDEA HUYU KIJANA!!!!!!!!!!!!!!!! Nimemaliza."
Previous Post Next Post