Mfanyakazi wa kampuni ya Wema Sepetu, Endless Fame Films, ambaye pia ni Meneja wa msanii, Mirror , Petit Man apo awali alidaiwa kuwa na uhusiano na Kajala, kisha kuwa na mdogo wake Vanessa Mdee, amethibitisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yake Diamond Platnumz, Esma na kwamba ana mipango ya kufunga naye ndoa.
“Ni kweli Esma ni mchumba wangu na Mungu akijalia soon tunafunga ndoa,” alisema Petit kwenye kipindi cha My Playlist kinachorushwa na Clouds TV. Alipoulizwa jinsi Diamond anavyouchukulia uhusiano wao, alisema: