Afungwa Jela kwa Kosa la kumpigia simu mpenzi wake wa zamani

Mwanaume mwenye umri wa miaka 33, raia wa Ufaransa amefungwa jela kwa kosa la kumsumbua mpenzi wake wa zamani kwa kumpigia simu mara 21,807 akimtaka amshukuru kwa kukarabati nyumba waliokuwa wakiishi.

Mwanaume huyo alikiri kufanya kosa hilo na kueleza kuwa ulikuwa ‘upumbavu’ kwa kuwa alikuwa amekatazwa kuwasiliana na mpenzi wake huyo wa zamani kwa kipindi cha miezi kumi iliyopita na akakubali.


Amehukumiwa kwenda jela miezi 10, huku miezi 6 ikisamehewa, na anapaswa kulipa fine ya £793).

Pamoja na kifungo hicho, ameamriwa kuhudhuria matibabu maalum ya akili na marufuku ya kuwasiliana tena na mwanamke huyo.

Mwanaume huyo aliwahi kulazwa hospitalini kutokana na msongo wa mawazo wakati akijaribu kuendana na hali halisi baada ya kuachwa na mpenzi wake huyo mwaka 2011.

“Muda ule, mantiki yangu ilkuwa hadi arudishe pesa nilizotumia kukarabati nyumba yetu…au angalau aseme ‘asante’, nisingeweza kuacha kumpigia simu.” Aliiambia mahakama ya Lyon.

Imedaiwa kuwa kwa siku moja mwanaume huyo alikuw akipiga simu na kutuma messages zaidi ya mara 73 kwa siku hali iliyogeuka kuwa usumbufu mkubwa.

Via: TheGuardian London
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa