Wema Sepetu kuendeleza Show yake ya In My Shoes mwezi September, na kitu kingine kikubwa kuja kutoka kwake 'Martin Kadinda'

Martin Kadinda amabaye ndiye meneja wa Wema Sepetu, amesema kuwa anatambua kuwa muigizaji huyo hajafanya kitu kikubwa mwaka huu kutoka kwenye kampuni yake ya Endless Fame Films, lakini amewataka watanzania kukaa mkao wa kula mwishoni mwa mwaka huu.




“Kuna vitu vingi ambavyo Wema anavifanya, so far show inarudi mwezi September ‘In My Shoes’ , something big Wema anafanya mwisho wa mwaka huu,” amesema Kadinda.

“Kweli Wema hajafanya vitu karibuni lakini watu wasubiri mambo makubwa, hajaamua tu kukiweka kwenye media, mpaka vitu vinavyotakiwa vikishawekwa sawa.Sometime huwezi kuongea jambo ambalo hata halijafikia asilimia 50 ya jambo. Endless Film ipo na kuna jambo ambalo kama kampuni Wema anatakiwa afungenalo mwaka ambalo is something big, kwahiyo watu wasubirie wataona nini Wema amekifanya, ” Martin ameongeza.
Previous Post Next Post

Popular Items