Video: Floyd Mayweather ashindwa kusoma jingle ya kipindi cha The Breakfast Club, mtazame hapa

Alhamisi iliyopita, 50 Cent alipost kipande cha video akimchallenge Floyd Mayweather Jr kusoma kwa sauti ukurasa mmoja tu wa kitabu cha Harry Potter, hali iliyoibua hisia tofauti kuhusu uwezo wa Mayweather katika kusoma.



Challenge ya 50 Cent ilikuwa sehemu ya kampeni ya kutoa msaada kwa wagonjwa na taasisi zinazohudumia wagonjwa wa ALS ambayo inaendeshwa kwa kujimwagia ndoo ya barafu, lakini yeye alitaka kuifanya tena tofauti akiahidi kutoa mamilioni endapo Mayweather akifaulu mtihani huo.

Kipindi cha The Breakfast Club kimepata sauti ya bondia huyo alipokuwa akiingiza drop/jingle katika kituo cha radio cha Power 105.1.

Katika kipande hicho cha sauti Floyd anasikika akihangaika sana kusoma sentensi mbili tu za drop hiyo.

Iangalie video hii kumsikiliza:



Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA