Sitti Mtemvu ndiye aliyetwaa taji la Miss Temeke 2014,

Shindano la kumtafuta mrembo wa Temeke, Miss Temeke 2014 yalifanyika juzi usiku katika ukumbi wa TCC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo Sitti Mtemvu aliibuka mshindi.Sitti Mtemvu alilivaa taji hilo na kuwa mshindi wa kwanza huku mrembo Salama Saleh akishika nafasi pili, na Neema Mollely alitajwa kuwa mshindi wa tatu.


Matokeo hayo yanawapa warembo hao watatu tiketi ya kuwa wawakilishi wa Wilaya ya Temeke katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania 2014).

Shindano hilo lililokuwa na washiriki 17 lilishereheshwa na Gardener G. Habash,  lilipambwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali akiwemo TID na Young Suma.

Tazama picha kadhaa kutoka kwenye shindano hilo..







Previous Post Next Post