'The Industry' ndio studio mpya ya Nah Real, Diamond Platnumz aibariki

Mtayarishaji wa muziki, Nahreel amefungua studio mpya iitwayo ‘The Industry’ na tayari amefanya wimbo na wasanii mbalimbali wakiwemo Diamond, Nikki wa Pili pamoja na kundi lake, Navy Kenzo.




Nahreel amesema studio hiyo ina wiki moja tu tangu ifunguliwe lakini tayari imeshafanya nyimbo na wasanii kadhaa.

“Yeah kuna kitu kinaendelea Diamond alikuwa kwenye studio yetu mpya The Industry, pia kuna ngoma nyingi nimeshafanya, toka nimefungua nadhani ni wiki moja na kazi nyingi tayari nimeshafanya. Nimefanya kazi na Nikki wa Pili nisingependa kuizungumzia, Diamond, Navy Kenzo pia tunatarajia kutoa nyimbo mwezi wa kumi tayari nyimbo zetu tumefanya tayari kwa muda mfupi huu, " Nahreel ameiambia tovuti ya Bongo5.

Nahreel amesema sababu ya kuipa studio yake jina la 'The Industry' ni kutokana na mchango wake kwenye industry ya muziki wa Tanzania.

"Mimi ni part of industry na industry yetu ya muziki nimeplay part kubwa, kwahiyo nikaona studio ikiitwa The Industry itakuwa imejumlisha vitu vingi. Halafu The Industry itakuwa the big company itakuwa inarekodi, itafanya photo shoot na baadaye inaweza ikaanza kufanya video. Kwahiyo ni kampuni ambayo itakuwa inakua kutokana na muziki ulivyo.”
Previous Post Next Post