Hivi ndivyo jinsi mkungenzi wa Vodacom alivyomwagiwa maji kuchangia Fistula Tanzania, #FistulaIcebucketChallenge

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza akishiriki #BongoIce challenge kwa lengo la kuchangisha fedha kugharamia matibabu ya ugonjwa wa Fistula ambao umekuwa tishio kwa kinamama. #ALSIceBucketChallenge


Kampeni hii imenzishwa na Vodacom kwa kutumia mfano wa kampeni maarufu iliyoanzishwa nchini Marekani kwa ajili ya kuchangia utafiti wa matibabu ya ugonjwa wa ALS iliyopewa jina la ALS Ice bucket Challenge.



Mkurugenzi huyo wa Vodacom ameeleza kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuchukua mfano wa ALS Challenge iliyoshika kasi kwenye mitandao ya kijamii, kwa kuzingatia kuwa akina mama wajawazito zaidi ya 30,000 wanaugua ugonjwa wa Fistula kwa kukosa huduma bora za matibabu.

Amewataja (nominate) Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba, Mkurugenzi wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel, Sunil Colaso.
Previous Post Next Post