Shilole atumia tsh Mill 13.3 kushoot video ya Namchukua

Muimbaji na Muigizaji wa filamu , Zuwena Mohamed aka Shilole amesema video ya wimbo wake mpya ‘Namchukua’ iliyoongozwa na Mkenya Kelvin Bosco Jr, imemgharimu dola 8,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 13.




Shilole alikuwa akizungumza na mtangazaji wa Mbeya Highlands FM, Elly.

“Video imefikia hatua za mwisho kabisa kumalizika huko nchini Kenya, Nairobi, nategemea fans wangu wataiona soon kwenye video zao,” alisema. “Imenigharimu pesa nyingi sana, kama dola elfu nane. Nimeamua kubadilisha ladha baada ya kufanya na directors wengi wa hapa Tanzania. Hapa nimefanya kama video saba hivi sasa nikaona bora nijaribu kubadilika kidogo tutafute ladha tofauti ndio nikaamua kufanya na mshikaji Kelvin Bosco.”
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa