Robin Williams ameacha filamu 4 alizoigiza na hazijatoka

Muigizaji kipenzi cha wengi Robin Williams kutoka Hollywood aliyefariki dunia Jumatatu asubuhi (Agosti 11) baada ya kujiua kwa kujipiga kitanzi, ataendelea kuonekana katika filamu nne alizokuwa amecheza kabla ya kifo chake ambazo bado hazijatoka.


Filamu hizo ni ‘Night at the Museum: Secret of the Tomb,’ ‘Merry Friggin’ Christmas,’ ‘Boulevard,’ pamoja na ‘Absolutely Anything.’

Kabla umauti haujamfika Williams alikuwa amemaliza kurekodi role yake katika filamu ya comedy ‘Merry Friggin’ Christmas,’ inayotarajiwa kuanza kutoka mwezi Novemba na kufuatiwa na ‘Night at the Museum: Secret of the Tomb’ iliyopangwa kutoka Desemba mwaka huu.

Studio ya 20th Century Fox wanohusika na filamu hizo wameelezea pengo lililoachwa na Williams.

“There really are no words to describe the loss of Robin Williams, He was immensely talented, a cherished member of our community, and part of the Fox family. Our hearts go out to his family, friends and fans. He will be deeply missed”.

Source: CNN
Previous Post Next Post