Picha: Serengeti Fiesta Bukoba ilikuwa kama hivi, full burudani

Tamasha la Serengeti Fiesta linalodhaminiwa na kinywaji mashuhuri cha Premium Serengeti linaendelea huku likitoa murua katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.

Hizi ni baadhi ya picha za tamsha hilo.


Winfrida Josephat 'Rachel' akitoa burudani katika Tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo, Bukoba.


Msanii wa kundi kijulikanacho kama International, Moses Nyama akiwaongoza wenzake wakati wa onyesho la

Serengeti fiesta 2014, lililofanyika jana jioni Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba


“Umati ulikuwa mkubwa sana…tiketi ziliisha mapema na ikatuladhimu kutafuta njia za kupata tiketi nyingine ili kila mwana Bukoba aliyefika uwanjani apate fursa ya kushuhudia burudani ya kweli,” alisema Meneja wa bia ya Serengeti, Rugambo Rodney.
Ommy Dimpoz’,akiwapa mkono baadhi ya mashabiki wake katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni

Uwanja wa Kaitaba ulizizima kwa shangwe pale mototo wa nyumbani, Saida Kalori alipopanda jukwaani huku akiporomosha burudani ya asili.
Msanii maarufu wa nyimbo za asili, Saida Karoli, akilitawala jukwaa wakati wa onyesho la Serengeti Fiesta
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi. Khamis Kagasheki (kulia), akimpongeza mmoja wa wasanii walioshinda katika Mashindo yaliyojulikana kama dansi la Serengeti fiesta 2014, Joylen Hamis, wakati wa tamasha la Serengeti fiesta kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba

Kwa mujibu wa Serengeti, kundi hili la wasanii lililotoa burudani Bukoba ndilo lItakalokwenda kushusha mvua ya burudani huko Kahama siku ya Jumapili. Tamaha la burudani la fiesta Bukoba liliambatana pia na shindano la kuimba lililowashirikisha wasichana wadogo lijulikanalo kama Serengeti SupaNyota Divas.

Barnaba Boy akitumbuiza kwenye uwanja wa Kaitaba

Mshindi aliyepatikana Bukoba ataambatana na washidi wengine jijini Dare es Salaam ili kumpata mshindi wa mashindano hayo mwaka huu. Baada ya Mwanza, Bukoba tamansha hili litaelekea mjini Kahama, na baada ya kahama, burudani hili la nguvu litashuka mikoa mbalimbali kama Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Tanga, Moshi, Arusha, Mtwara na Dar es salaam na hatimaye jijini Dar es Salaam ifikapo oktoba 18 mwaka huu

Mmoja wa wasanii waliong’ara katika tamasha la Serengeti fiesta lililofanyika juzi, Ney wa Mitego akikonga nyoyo za mashabiki katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni.
Ommy Dimpoz akitumbuiza kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba
Ikidumisha kasumba yake ya kutoa burudani halisi kwa wapenzi wake, Premium Serengeti iliwapeleka wasanii mashuhuri kutoka pande zote nchini. Ilipofika majira ya saa kumi jioni, uwanja wa Kaitaba ulikuwa umefurika mashabiki kutoka pande mbalimbali wakisaka tiketi za kuingilia ukumbini.
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mama Zipora Pangani wakati wa tamasha la Serengeti fiesta katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
DJ Fetty akifanya yake.
Mashabiki waliojitokeza katika Serengeti Fiesta Bukoba.

Jux akiimba wimbo wake mpya wa Nitasubiri.
Mtoto wa Saida Kaloli akicheza ngoma.

Saida Karoli akiwanyanyua mashabiki wake.
Stamina akifanya yake jukwaani.

Credit:Bongo5/Gpl
Previous Post Next Post