Chris Brown na Trey Songz watangaza kufanya tour ya pamoja, uwachagulie wewe jina

Waliokuwa mahasimu wasio rasmi, wakali wa R&B Chris Brown na Trey Songz ambao waligeuka kuwa washikaji mwaka huu na kupanda jukwaa moja wameamua kufanya biashara ya pamoja.

Wasanii hao wametangaza kupitia Instagram kwa kupost videos wakiwaeleza mashabiki kuwa wameamua kufanya tour ya pamoja ambayo wote wameisifia.



Chris Brown amewaahidi mashabiki wake kuwa katika tour hiyo watapata R&B na performance ya kweli.

Wasanii hao wamewataka mashabiki wawasaidie kupata jina la tour hiyo ambayo bado haijapata ratiba rasmi.

“THIS FALL is gonna be legendary! Get ready for me and @TreySongz Tour!!!!!!” Ametweet Chris Brown.
Mara ya mwisho wakali hao waliimba pamoja katika jukwaa la tuzo za BET, June mwaka huu wakiwa na August Alsina.


Previous Post Next Post