Picha: Professor Jay afanya video yake nyingine ya chafu 3 na director kutoka kenya .

Safari hii Joseph Haule aka Professor Jay ni kama ameamua kulipa deni alilonalo kwa mashabiki wake, sababu amesema hataki kuweka gap la ukimya tena, itakuwa ni mwendo wa bandika bandua.


Baada ya kutoa single ya ‘Kipi Sijasikia’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz mwezi April, hivi karibuni ameachia audio ya single nyingine inayoitwa ‘Tatu Chafu’.

Licha ya kuwa video ya ‘Kipi Sijasikia’ aliyoshoot na Adam Juma wa Visual Lab: Next Level mwezi uliopita (July) bado haijatoka, tayari ameanza kushoot video ya single mpya ‘Tatu Chafu’ chini ya mwongozaji Hefemi.

Kupitia Instagram Jay ameshare picha za BTS ya utengenezaji wa video ya ‘Tatu Chafu’

“Day one. .. Madirector na maproducer wetu tukiwawezesha WANAWEZA , Asante Mungu. .. #Hatuachii Gap #Nakung’ata mchana kweupeee kama MBU wa DENGU #puna Nikupune #BACK2BACK MUZIK #STRICKLY HIPHOP #TheMastermind of the GAME #Nilimshawishi baba yako akuruhusu Uimbe. ..UNABISHA??? @hefemi @nkwabi1 @adamjumanxl @nisherbybee @majani187 @marcochalitz @fresh120media” Aliandika Professor Jay




Previous Post Next Post