Picha: Kilichoenedelea jana katika shoo ya Tamasha la Usiku wa Matumaini iliyofanyika Uwanja wa Taifa

Katika siku ya jana, Pale uwanja wa Taifa lilifanyika Tamasha la Usiku wa Matumaini, Tamasha limefanyika jana katika uwanja wa Taifa na kuudhuriwa na Mashabiki kibao kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam. Burudani kali zilikuwepo katika Tamsha hilo ikiwa ni pamoja na Mapambano ya Ngumi na mengine mengi.



Wasanii waliokuwepo walitoa Burudani ya kufa mtu ambayo iliwafanya mashabiki wazidi kupiga Kelele kwa Furaha, Mbali na wasanii kutoka Tanzania alikuwepo Mwanadada Kutoka Nchini NIGERIA 'Yemi Alade' ambaye anatamba na kibao chake cha Johny  mbali na yemi alade kutoa Shoo kali wasanii wa Bongo nao walipagawisha vya kutosha

Tazama picha zaidi hapa chini.. Video itafuata


Yemi Alade akipiga shoo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 Ahmad Ally 'Madee' akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.





Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi wakifanya yao ndani ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 Uwanja wa Taifa.
Nature akiwadatisha mashabiki wake.
Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi wakifanya vitu vyao.


Previous Post Next Post

Popular Items