Mtoto wa Jackie Chan hatiani kwa matumizi ya dawa za kulevya, anaweza kufungwa miaka 3

Mtoto wa kiume wa muigizaji wa filamu za Hollywood, Jackie Chan amekamatwa kwa makosa ya matumizi ya dawa za kulevya.


Jaycee Chan

Jaycee Chan, 31, ambaye pia ni muigizaji pamoja na staa mwingine wa filamu wa Taiwan, Kai Ko, 23, walikamatwa Alhamis iliyopita. Polisi wamedai kuwa wote wawili walipimwa na kubainika walikuwa wamevuta bangi na pia zaidi ya gram 100 za dawa za kulevya zilikutwa nyumbani kwa Chan.


Jaycee Chan na rafiki yake Kai Ko

Kama akipatikana na hatia, Chan atafungwa jela kwa miaka mitatu.
Previous Post Next Post

Popular Items

HOW TO LOOSE GOOD WOMAN

5 THINGS YOU DON'T KNOW ABOUT LIL COOL J