Mpenzi wa Criss Brown 'Karrueche Tran' aomba radhi kwa utani alioutoa kwa mtoto wa Beyonce, Blue Ivy

Mpenzi wa Chris Brown, Karrueche Tran amejikuta akishambuliwa vikali na mashabiki wa Beyonce baada ya kufanya utani kuhusu nywele za mtoto wa Jay Z na muimbaji huyo, Blue Ivy.

Mrembo huyo aliongea utani huo kwenye kipindi cha 106 and Park cha BET Jumatatu juu. “I really did wake up like this because my parents never comb my hair,” alisema Karrueche kama utani wa mambo ambayo wanadhani Blue alikuwa akiwaza wakati wa tuzo za MTV VMA.




“Sorry, Blue I love you,” alimalizia Karrueche bila kuwa na wazo jinsi utani huo ulivyowachukiza wengi.

Mashabiki wa Beyonce maarufu kama BeyHive wamemshambulia mrembo huyo kwa matusi na kumtolea vitisho vya kumuua.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Karrueche aliandika:

“Past two days have been extremely draining.. As I geared up for a big day for myself – hosting a live show.. I never expected things to turn out this way.. I apologize to any and everyone who felt offended in any way by the comments made by BET executed through me.. I would never disrespect anyone’s child in any way and anyone who knows me knows that I LOVE Beyoncé. My comments have been in complete shambles.. yes I am human too and yes I do make mistakes.. But all this negativity and death wishes are quite a lot.. Definitely a lesson learned from here forth.. Again, on behalf of MYSELF, my sincerest apologies ❤️ #BeyHive”.

Naye Mkurugenzi wa BET, Stephen G Hill amewaomba radhi watu waliokwazwa na utani huo aliouita wa kijinga na kumtetea Karrueche huku akiahidi kuwachukulia hatua kali waliohusika. BET pia imewaomba radhi Jay Z na Beyonce.
Previous Post Next Post