Video Interview: Nuh Mziwanda, Shilole amenifanya nione mwanga kwenye gemu ya BongoFleva

Mwanamuziki na mpenzi wa Shiloe Kiunowa Bongo Fleva, Nuh Naftari Mlawa ‘Nuh’ amefunguka ya moyoni kuhusiana na kipaji chake na kusema kuwa ‘sexy lady’ wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ndiye aliyempa mwanga kunako gemu ya Bongo Fleva.

Akizungumza kupitia Global TV Online , Mziwanda alimshukuru Shilole na kuongeza pia kujichora kwake mchoro mkononi wenye jina la bidada huyo ni kuweka historia kuwa alishawahi kutokea mtu wa muhimu maishani mwake.

“Zamani nilikuwa nafanya muziki lakini nyota yangu haikung’aa kihivyo, baada ya kumpata Shilole nyota zetu zikaonekana kuwa sawa hivyo nikang’aa japo mapenzi ndiyo yaliyotuunganisha,” alisema Mziwanda.

Tazama hapa kihojiwa..

Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA