Maswali 10 ya kujiuliza kabla aujaachana na mpenzi wako

Leo tunazungumzia  kuhusu maswali ya kujiuliza kabla ya kuachana inaendelea! Ina maana kubwa sana endapo utaelewa hoja zake na kuamua kuzifanyia kazi. Nilishaeleza mwanzoni kuwa uhusiano wowote huanza kwa furaha na matarajio mengi. Siku zinavyokwenda mambo hubadilika.

yanapochukua nafasi hufanya tamu kugeuka shubiri. Wanafasihi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ waliimba katika wimbo wao Sumu ya Mapenzi kwamba “sumu ya mapenzi ni maudhi”.
Kwamba, maudhi yanapoingia kwenye uhusiano huigeuza ladha ya asali kuwa shubiri. Humsababishia mtu kumuona mpenzi wake ni mbaya kama Shetani wakati mwanzoni alimsifu kuwa ni mzuri mithili ya malaika. Hii ni namna ambavyo mapenzi yanaweza kubadilika.



Binadamu wametofautiana, wapo wenye mioyo yenye matarajio ya kuendelea, vilevile kuna wenye matarajio ya mgeuko au mabadiliko. Sitaki kutumia nyoyo ngumu kwa maana hata yule anayesemwa ana moyo mgumu huumia, pengine zaidi ya anayeitwa mwenye moyo mwepesi.

Mwenye moyo wenye matarajio ya kuendelea anakuwa na imani kwamba hata baada ya migogoro mingi na mwenzi wake, lipo penzi la kweli na maisha yenye furaha zaidi na upendo baadaye. Kwa maana hiyo husamehe akitarajia kupata kilicho bora baada ya misukosuko.

Aliye na matarajio mgeuko au kwa lugha nyingine anayeamini mabadiliko, baada ya maudhi na migogoro hushindwa kuvumilia. Imani yake humwambia kwamba akipata mpenzi mwingine, anaweza kuishi maisha ya furaha na maelewano zaidi kuliko kuendelea na aliyenaye.

Katika mada hii, tunajenga nyoyo zinazoweza kuishi kimapenzi hata baada ya migongano. Ni suala la kuketi na kujiuliza vitu kadhaa kabla ya kupata jawabu la kushika. Umeshajiuliza maswali matatu, sasa usiache kujiuliza na hili;

UNAJUA JINSI YA KUWASILIANA NA MWENZI WAKO?
Katika kipengele hiki, anza kwa kujiuliza, “je, mimi na mwenzi wangu tunaelewana?” Jawabu litakuwa sababu ya kujisahihisha. Maisha ni kama kioo, ukiyachekea nayo yanacheka, ukiyawekea mgomo ndivyo nayo yatakavyokugomea, vivyo hivyo katika uhusiano wako.

Watu wanaoishi vizuri kwenye uhusiano wao, wanaowasiliana na kuelewana, daima uhusiano wao huwa hauendi na maji. Nisisitize kitu kwamba sio kuwasiliana, bali kuwasiliana na kuelewana! Wapo watu wengi wanaowasiliana, tena vizuri kabisa lakini hawaelewani.


kuachana na mwenzi wako ni vizuri uwe umeshajiuliza swali hili kama unajua namna bora ya kuwasiliana naye. Swali la pili linakuwa “je, tunaelewana?” Kama mawasiliano yenu hayana maelewano ni vizuri kuanza kusuka upya mawasiliano yenu. Lazima uwe na jibu la namna ambavyo mkiwasiliana mnakuwa mnaelewana.

Kama mpenzi wako hakuelewi, jiulize kwa nini hueleweki? Ni wajibu wako kufanya juu chini ili mwenzio akuelewe. Kwa kifupi ni kwamba maelewano ni hali ya kupokea na kutoa, yaani yeye akuelewe na wewe umuelewe. Hakuna kitu kinachoitwa maelewano ya upande mmoja.

Jifunze namna bora ya kuwasiliana na mwenzi wako, naye mfanye ajue kuwasiliana na wewe. Baada ya hapo, utakuja kugundua kwamba kumbe hakukuwa na sababu yoyote ya kuachana, yalikuwa ni mapito yaliyohitaji kutuliza kichwa chini na kusuka upya utaratibu. Usilisahau swali hili!

JE, UNAJUA TOFAUTI YENU KIJINSIA?
Mwanamke na mwanaume hawawezi kuwa sawa. Kimaumbile umetofautishwa sana na mwenzi wako. Hilo unapaswa kulitambua. Kama hili utalijua vizuri na kulifanyia kazi, kwa hakika utakuwa mwenye subira sana. Utaweza kumrekebisha mwenzi wako kwa njia inayokubalika.

Kuna udhaifu wa kiasili ambao upo ndani ya mwanaume. Ukisema mwenzi wako hakufai na ukaamua kuachana naye bila kufanya uchunguzi na kugundua kwamba kasoro zake zipo nje ya udhaifu wake kama mwanaume, utakachokipata ni kuwa utakayempata baadaye si ajabu ukavuna yaleyale.

Kwa kawaida wanawake wanayo mapungufu yao kiasili, usije kuachana na mwenzi wako kwa sababu ambazo zipo ndani ya mapungufu hayo. Hakikisha unajua tofauti ya kijinsia na udhaifu wa jinsi ya pili. Hakuna kosa kubwa linaloweza kukuumiza baadaye kama kugundua kwamba uliachana na mwenzi wako kimakosa.
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa