Young Killer kuja na 'umebadilika' ni wimbo mpya atakaouachia Jumanne

Rapper toka Rock City Mwanza, Young Killer amepanga kuachia wimbo mpya aliupa jina la Umebadilika ikiwa ni wiki moja tangu alipoachia video ya ‘My Power’.

Rapper huyo ameeleza kuwa wimbo huo utakuwa tofauti na nyingi walizozizoea kutoka kwake.



“Ngoma ni ya tofauti kidogo. Ujio wangu wa round hii..itakuwa ni ngoma ambayo inahitaji mtu akae awaze kwa sababu ni ngoma ambayo nimeiandika kwa utulivu. Hata watu pia niliofanya nao na production ambayo nimefanya nayo nikiwaambia mtu lazima ashtuke kidogo. Ni ngoma Fulani ya utulivu inaitwa ‘Umebadilika’.”

Amesema mdundo wa wimbo huo umetayarishwa na Dee Classic wa Mwanza lakini Vocal na mixing amefanya Man Walter wa Combination Sound.
Previous Post Next Post