Huu ndio mkwanja aliolipwa Producer Tudd Thomas katika kutengeneza Mdogo Mdogo ya Diamond Platnumz na Ndagushima ya Ommy Dimpoz

Mtayarishaji wa muziki Tanzania Tudd Thomas ndiye aliyetayarisha wimbo wa Diamond ‘MdogoMdogo’ ambao unafanya vizuri sana pamoja na wimbo wa Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’ ambazo zote zimepata nafasi kubwa huku wasanii hao wakilipa mamilioni kufanya videos.



Akiongea wakati akiojiwa katika kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm na Fadhili Haule, Tudd amesema kuwa alilipwa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila wimbo katika nyakati tofauti.

“Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.” Alisema.

Ameeleza kuwa gharama za nyimbo hizo zilitokana na ukubwa wa nyimbo zenyewe na muda alioutumia kukaa studio na wasanii hao.
Previous Post Next Post