Video: Mwanadada Iggy Azalea apata shavu kwenye Fast and Furious 7

Hizo ndizo updated news za Fast and Furious 7 Mwanadada Iggy Azalea anazidi kufanikiwa. Kutoka kwenye ‘Fancy’ na sasa kwenye filamu ya ‘Fast & Furious.


Rapper huyo wa Australia ataonekana pamoja Vin Diesel kwenye Fast & Furious 7. Kwenye filamu iliyopita ya Fast and Furious, Rita Ora alipewa shavu la kuonekana. Habari hiyo imetangazwa na Vin Diesel wakati akijibu swali kwenye interview aliyofanyiwa na Skyrock FM.



Fast & Furious 7 inatarajiwa kuingia sokoni April 3, 2015 ikiwa na waigizaji kama Ludacris, Tyrese, Dwayne Johnson, Michelle Rodriguez na marehemu Paul Walker.



Pamoja na hivyo, Iggy alichaguliwa kuwa mtangazaji wa show ya MTV, “House of Style,” itakayoanza kuoneshwa August 4 kupitia MTV.com. Hivi karibuni pia alitajwa kuwania vipengele 7 MTV Video Music Awards.

Previous Post Next Post

Popular Items