Ujerumani ndio mabingwa wa kombe la dunia Brazil 2014




Mabingwa wa kombe la dunia Brazil 2014 NI Ujerumani

Mario Götze anaipatia Ujerumani bao la ushindi.

Ujerumani wanakuwa timu ya kwanza ya kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika mchuano ulioandaliwa Kusini mwa Marekani.

Ujerumani ilihitaji bao la muda wa ziada la Mario Gotze kuinyamazisha Argentina katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Maracana.

Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.



Kipa Nuer wa Ujerumani alituzwa ''Golden Glover'' Huku Messi akituzwa kama mchezaji bora 'Golden Ball'' Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''.
Ijapokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo la ''Golden Ball''.

Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.



Rais wa Urusi Vlamir Putin alipokea ithibati rasmi ya kuandaa makala yajayo ya kombe la dunia kutoka kwa rais wa FIFA na rais wa Brazil.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwepo Maracana kwa mualiko wa rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Brazil Dilma Rousseff.

Putin alipewa ithibati rasmi ya kuwa mwenyeji wa makala yajayo ya kombe la dunia la mwaka wa 2018.

00:25 Mario Gotze anaiweka Ujerumani mbele

00:24 GOOOOOOOOAL

00:08 Palacio anapoteza nafasi nyengine huku Messi akionekana kulemewa na walinzi wa Ujerumani.




Argentina imehifadhi timu iliyoilaza Uholanzi katika nusu fainali

Je Historia itajirudia ?

Argentina nayo inakumbuka vyema matukio ya miaka 28 iliyopita ilipoilaza Ujerumani Magharibi wakati huo na kutwaa kombe lao la mwisho la dunia

Ujerumani ilishinda mara moja nayo Argentina ikaibuka mshindi mara moja kwa hivyo hii leo itakuwa mechi ya kukata na shoka .

Wajerumani wakiandikisha rekodi kwa kuinyeshea wenyeji Brazil jumla ya mabao 7-1 katika nusu fainali huku Argentina nayo ikihitaji muda wa ziada na hata mikwaju ya penalti kuibandua Uholanzi na kufuzu.



Timu ya Ujerumani ikifanya mazoezi

Ujerumani itakuwa timu ya kwanza kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika Marekani ya kusini iwapo itaipiku Argentina.

Timu hizi zimechuana mara 2 katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 1986 na 1990.



Mahasaimu wa Jadi Argentina wanachuana na Ujerumani katika fainali yao ya tatu katika historia ya kombe la dunia.

Macho yote duniani yanaelekea katika uwanja wa Maracana ulioko Rio Brazil ambapo mechi ya fainali ya kombe la dunia itachezwa muda mchache ujao.

Jumapili ya tarehe 13 Julai mwaka wa 2014 hatimaye imewadia .



Uwanja wa kihistoria wa Maracana

Katika mechi hii ya leo Mahasimu hawa wanafahamiana sana.

Hayo yote ni kenda timu hizo zote zilikuwa zikiwania kuandikisha majina yao kwenye tuzo la kipekee la dhahabu yaani kombe la dunia.

Mechi hiyo ndiyo itakayokuwa kilele cha majuma manne ya kipute hicho kilichojumisha timu 32 kutoka mabara yote 5 zikichuana miongoni mwao katika miji 12 ya Brazil kuanzia juni tarehe 12 .




Shamrashamra za kufunga makala ya mwaka huu tayari yameanza

Argentina wakiwa wamevalia sare ya samawati Ujerumani ikiwa na Jezi Nyeupe .

Timu zimeingia uwanjani tayari kwa fainali hii.

Wimbo wa taifa wa Ujerumani unapigwa kisha ule wa Argentina .

Vijana wa Joachim Loew wanamtarajia mfungaji wao nyota Miroslav Klose akisaidiana na Thomas Muller kuwapa mabao na hatimaye ushindi dhidi ya Argentina .

Kwa Upande wao Ujerumani imesifiwa kwa kuwa na uwezo wa kipekee wa kucheza kama kikosi wala sio kumtegemea nyota mmoja kwa ufungaji mabao.



Argentina 0-0 Ujerumani 10''

22:05 Ujerumani 0- 0 Argentina

22:03 Argentina wanashambulia lango la Ujerumani lakini wapi .

22:01 Freekick kuelekea lango la Argentina .

22:00 Mpira umeanza .



Ujerumani 0- 0 Argentina 20''

22:45 Halftime .Ujerumani 0-0 Argentina

22:45 Ujerumani wanapoteza nafasi nzuri mkwaju wa kichwa unapogonga mwamba na msaidizi wa refarii anasema ni Offside kwa Thomas Muller

22:39 Lionel Messi ananyimwa fursa ya kufanya mashambulizi

22:37 Ujerumani wanafanya shambulizi lingine .

22:35 Higuan anafunga lakini refarii anakataa anasema aliotea .

22:20 Gonzalo Higuan apoteza nafasi ya wazi akiwa amesalia pekee yake na na kipa Nuer

22:18 Ujerumani 0- 0 Argentina 20''

22:14 Kona kuelekea upande wa Argentina.

22:13Freekick kuelekea lango la Argentina lakini wapi unagongwa nje na unakuwa wa kurushwa kuelekea Argentina.

22:10 Kona ya kwanza katika mechi hii kuelekea upande wa Ujerumani

22:09 Messi anaongoza shambulizi hadi ndani ya eneo la lango lakini mjerumani hapishi.



Argentina 0-0 Ujerumani 37''

00:55 Nuer anambonda Higuain lakini refarii anasema ni Freekick kuelekea lango la Argentina

00:48 Goalkick kuelekea upande wa Argentina

00:46 Messi anapoteza nafasi nyengine

22:45 Sergio Aguero anaingia badala yake Ezequiel

22:45 Ujerumani 0-0 Argentina

22:45Kipindi cha pili kinaanza huko Maracana



Argentina 0-0 Ujerumani 90''.

00:87 Miroslav Klose anaondoka

00:86 Joachim loew anajibu kwa kumuingiza Gotze

00:85 Argentina inajiandaa kufanya mabadilikokatika safu ya kati Gago anaingia



Argentina 0-0 Ujerumani 65''.

00:65 Kadi ya njano Mascheranona na Aguero

00:60 Argentina 0-0 Ujerumani 60''.

00:58 Argentina 0-0 Ujerumani




Mashabiki wa Ujerumani wakitangaza msimamo wao .

00:81 Argentina 0-0 Ujerumani 82''.

00:80 Krooooooooos anapoteza nafasi nyengine

00:70 Ujerumani inakosa tena Schurrle



Ujerumani 0-0 Argentina ExtraTime

Mechi imekwisha .
Argentina 0-0 Ujerumani 90''.
Sasa ni Muda wa Ziada (Extra Time)

00:90 Argentina 0-0 Ujerumani 90''.

00:90Muda wa kawaida umekamilika katika fainali hii .




Gotze aiweka Ujerumani mbele 1-0

00:02EXTRA Time imeanza .
Previous Post Next Post