Mwili wa mmiliki wa meli ya Korea Kusini wapatikana, alikimbia baada ya ajali na kufia mafichoni

Polisi wa Korea kusini wamethibitisha kuwa mwili walioupata mwezi June ni wa mmiliki wa meli iliyozama mwezi April na kuua watu zaidi ya 300 ambapo wengi wao ni wanafunzi.



Billionaire huyo anaefahamika kwa jina la Yoo Byung-eun alipotea muda mfupi baada ya meli yake kupata ajali na inadaiwa kuwa alikuwa anakwepa kukamatwa na kuhojiwa na polisi kama kuna uzembe wowote alioufanya na kusababisha kuzama kwa meli hiyo.



Msemaji wa jeshi la Polisi la Korea Kusini, Woo Hyung-ho amesema kuwa vipimo vya sampuli za DNA vimethibisha kuwa vimeendana na bwana Yoo aliyekuwa na umri wa miaka 73..

Previous Post Next Post