Linah awafungukia wsanii wa kike! aelezea wivu, majivuno na majungu yanavyowatafuna

Idadi ndogo ya wasanii wa kike Tanzania waliofanikiwa kimuziki na mbio za baadhi yao kuishia sakafuni husababishwa na mengi, lakini kumbe wao binafsi ni sehemu kubwa ya sababu za kuwapunguza kwenye mkondo mkubwa wa muziki.

Akiongea na Times Fm, msanii wa kike, Linah ambaye ni mmoja kati ya wasanii watano wa kike Tanzania wanaopiga hatua kubwa kimuziki na kuleta ushindani ameelezea wadudu wanaoshambulia maendeleo ya muziki ya wasanii wa kike Tanzania.



“Mimi nachoweza kusema ni wivu. Yaani sisi wasichana tuna wivu. Nakumbuka kuna wasichana kama wawili nilishawahi kuwafuata nikawaambia bana kuna wimbo huu hapa tufanyeje. Mtu aah sijui nini na nini…maneno pembeni ‘ah kwa sababu anaona mimi sasa hivi niko hivi na hivi’, yaani mambo kama hayo wasichana tunayo. Yaani hutaki mwenzio afanikiwe, unataka wewe tu ndio ukae na uwe wewe tu. Na ndio maana wasichana kwenye muziki tuko wachache kuliko wanaume. Yaani tuna ile tabia ya kwanini.” Ameeleza.

Amesema kwa upande wake alivyopata nafasi ya kwenda kufanya kazi Afrika Kusini alifikiria jinsi ya kuwavuta na wasichana wengine na kusafisha njia kama anavyofanya Diamond. Lakini badala yake wengi wameanza kumpiga majungu kuhusu safari yake.

“Kwa sababu kuna maneno nimeshayasikia, yaani hivi nakwambia nimerudi nasikia ‘oooh ana mabwana, sijui kapelekwa. Which is not true kwa sababu mimi niko kazini. Hata kama napelekwa niko kazini na kuna faida naipata. Wewe ambaye uko hapo na unafanya muziki umefanya kitu gani? Nimesaini mikataba mikubwa na kampuni kubwa na sio mchezo. Lakini mara ‘oh katika hayo makampuni aah mabwana’, unajua watoto wa kike. Kwa hiyo vitu kama hivyo vinaturudisha nyuma huwezi ukafanikiwa hata siku moja. Lakini ukivaa miwani ya bati ukasonga mbele basi unafanikiwa.” Amefunguka Asterina Sanga aka Linah.

Ameeleza kuwa wasanii wengi wa kike wa Tanzania hujivuna na ndio sababu ya kutokuwepo collabo za wasanii wakubwa wa kike.

“Angalia wenzetu Shakira na Rihanna wametoa wimbo unafanya vizuri, wanaonekana. Shakira na Beyonce walifanya wimbo. Sijui akina Kelly Rowland na wengine wengi. Hapa ulishasikia collabo ngapi za wasanii wakubwa wa kike kwa sisi tuliopo? Zaidi ya mimi na Khadija ambayo imetoka juzi.”




Amefafanua kuwa yeye aliamua kufanya wimbo na Khadija kwa sababu anaelewa kuwa yeye ni msanii mkubwa akifanya na msanii mpya wa kike na yeye atazidi kuwa mkubwa na ndio sababu hakuringa kama wengi wanavyofanya.

Linah ameachia kipande cha video yake mpya aliyoifanya Afrika Kusini na kampuni ya GodFather ‘ Ole Themba’.
Previous Post Next Post