Lil Wayne aanzisha kampuni ya usimamizi wa michezo na mteja wa kwanza ni Christiano Ronaldo

Mwanamuziki na mwanzilishi wa label ya Young Money Entertainment, Lil Wayne ameamua kuingia kwa miguu miwili kwenye michezo kwa kuanzisha kampuni ya usimamizi wa michezo.


Kwa mujibu wa TMZ, chanzo kimesema kampuni mpya ya Weezy tayari imeshapata mteja wa kwanza ambaye ni Christiano Ronaldo, ambayo itamsimamia shughuli zote za kimichezo kuanzia branding, endorsements, modeling hadi marketing kwa nchini Marekani.

kampuni mpya ya Weezy itakuwa ikifanya kazi na PolarisSports ambayo inauhusiano na CAA agency na GestiFute ambazo wakala wa Ronaldo Jorge Mendes anafanya nazo kazi.

Ronaldo amepost picha akiwa na waziri mkuu wa Japan na wanasiasa wengine wa Japan na wote wakionesha ishara ya YMCMB



Previous Post Next Post