Huu ndio ujumbe alioandika kajala kwenda kwa mwanae

Msanii wa filamu kajala Masanja leo (July 15) amemuandikia ujumbe mwanae Paula wasiku ya kuzaliwa kutokana na changamoto alizipitia wakati wa kumlea.


Kajala kupitia instagram amesema:Miaka 12 iliyopita sikuwahi kujua kama itafikia siku nitajisikia hiki ninachofeel siku ya leo.. nimepitia mambo mengi sana na wewe.. nimepata shida nyingi mno lakini sikukuacha wala kukutupa.. kwenye jua ama mvua, iwe usiku ama mchana katika mitihani yote niliyopitia nilikuwa na wewe tu mwanangu.. ulikuwa kama pochi yangu.. bila kujua kesho utakuwa NANI!! nilikupenda tangu siku ya kwanza nakuona.. nilikuthamini na kuahidi nafsi yangu kuwa nitakufa na wewe katika hali yoyote ile bila kujua wewe una hisia gani juu yangu… wala sikujua kama unaweza kuja kuwa faraja kwangu.. Paula!!! Mtoto wangu wa utotoni.. mtoto ambae nna historia kubwa na wewe.. LEO napenda kumshukuru sana MUNGU kwa kunipatia wewe.. sababu uwepo wako wa miaka 12 kwenye Dunia hii umenipa majibu yote ya maswali niliyokuwa najiuliza… Umekuwa faraja kubwa sana kwenye maisha yangu.. Pamoja na umri wako kuwa mdogo umeweza kusimama na mimi kwenye hali zote.. nimeshuhudia lililoniumiza likikuumiza pia.. umenifanya nione thamani yangu.. umenipa thamani kubwa sana kwenye maisha yako.. katika safari hii umenihakikishia kuwa nina mtu mmoja ambae hata Dunia nzima initenge na kunizomea.. YEYE ATABAKI KUWA NA MIMI!!! Tena kwa moyo mmoja na mapenzi… na mtu mwenyewe si mwingine yoyote.. ila ni WEWE mwanangu.. nakupenda sana Paula!! Na nakuombea MUNGU akukuze kwenye imani na akupe kila la kheri katika dunia hii.. nilikupenda jana ukiwa mikononi mwangu, ninakupenda leo ukiwa binti na naahidi kukupenda milele katika maisha yangu ukiwa kwenye hali yoyote ile.. ulikuwa wa kwangu na utaendelea kuwa wa kwangu mpaka mwisho wa maisha yangu.. HAPPY BIRTHDAY my daughter!!!! NAKUPENDA SANA

Previous Post Next Post