Baada ya kushinda tuzo za BET, Davido azungumzia collabo yake na Rick Ross pamoja na MeekMill

Idadi ya collabo za wasanii wa Afrika, hasa Nigeria na mastaa wakubwa wa Marekani zinazidi kuongezeka. Baada ya Wizkid kuthibitisha kufanya collabo na Chris Brown na Rihanna, P-Square na T.I, sasa mshindi wa tuzo 2 za MTV (MAMA) na BET 2014, Davido nae amefunguka kuhusu collabo yake inayokuja na marapper wakubwa wa Marekani.



Davido ameuambia mtandao NEW AGE exclusively kuwa, anatarajia kufanya collabo na bosi wa MMG, Rick Rozay pamoja na ‘label mate’ wake Meek Mill ‘soon’.

“For now I cannot reveal much, but I can definitely tell you that Rick Ross and Meek Mill are on the cards for collaborations.” Davido aliuambia mtandao huo.

Pia kupitia Facebook Davido ameandika:
“Hot new collaboration coming out.Are you guys ready to see this? #‎RickRoss‬ ‪#‎MeekMill‬ ‪#‎HKNGang‬ ‪#‎MMG‬” na kushare link ya habari hiyo.

Hivi karibuni Davido alipokuwa Marekani alipost picha akiwa na Meek Mill, so inaonekana huo ulikuwa ni mwanzo wa mipango hiyo mikubwa inayokuja.

Previous Post Next Post