Linah aelezea maana ya 'Ole Themba', na jinsi atakavyofanya kazi na kampuni yake mpya ya No Fake Zone Entertainment

Mwanadad Linah amefunguka na kuleza maana ya‘Ole Themba’ ni jina la wimbo wa Linah ambao hivi sasa umepata nafasi sana kwenye vyombo vya habari na umekubalika na wengi kwa ubora wa audio na video. Lakini maana na alichokimaanisha moja kwa moja ni kitendawili kwa wengi.

Msanii huyu wa kike ameongea na Bongo Dot Home ya Times Fm na kueleza maana ya wimbo ambao umepewa jina la lugha ya Kizulu ‘Ole Themba’.



“Hiyo Ole Themba ni Kizulu, na maana yake ni tumaini. Kwa hiyo Ole Thembana maana yake ‘tumaini langu’ hicho ndicho nilikuwa nakimaanisha. Lakini all in all inahusu mapenzi, namwambia mpenzi wangu kuwa yeye ndiye tumaini langu na nini. Nampetipeti waswahili wanasema namjaza yaani” Amesema Linah.

Ameongeza kuwa melody na jina la wimbo huo alipewa na Uhuru wa Afrika Kusini, sehemu aliyorekodia.

Akizungumzia jinsi atakavyofanya kazi na kampuni yake mpya ya No Fake Zone akiwa kama msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kufanya kazi na kampuni hiyo, atakuwa anafanya kazi akiwa Tanzania na kwamba recording na mambo mengine yatamlazimu kwenda Afrika Kusini kuyakamilisha.

“Ile kuagwa nilikuwa naagwa hapa katika kikundi nachofanyia kazi lakini NFZ wapo kote, wanabranch yao hapa Tanzania na ndio maana imekuwa rahisi kufanya kazi na mimi. Na nimekuwa msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kwa Afrika Mashariki. But it’s an International company.”
Previous Post Next Post