Usher na mtangazaji wa E! Entertainment TV ya Marekani kuja Tanzania July kuwapa semina wasanii wa muziki na filamu

Miongoni mwa vitu vitakavyofanya Rais Jakaya Kikwete akumbukwe na wasanii wa Tanzania ni jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wasanii katika kipindi chake cha uongozi.

 Usher
Sina shaka umeshasikia kuwa Rais Kikwete hivi karibuni alipokuwa Marekani alikutana na hit maker wa ‘Number 1’ Diamond Platnumz, na akamuunganisha na mmoja wa wadau muhimu katika muziki duniani Kevin Liles, ambaye ni meneja wa Trey Songz ili amsaidie.



Rais Kikwete alimpomkutanisha Diamond na Kevin Liles
Hivi sasa Mr President ametoa shavu lingine kwa wasanii wote wa muziki na filamu kwa kuwaletea wadau muhimu katika tasnia ya sanaa duniani, akiwemo muimbaji maarufu wa Marekani Usher pamoja na mtangazaji wa E! Entertainment Television, Terrence Jekins aka Terrence J.

Kevin Liles na Trey Songz
Akizungumza katika tamasha la uzalendo (Naiaminia Tanzania) Jumamosi iliyopita mjini Dodoma, Rais Kikwete amesema alipokuwa Marekani alikutana na watu muhimu katika sanaa duniani ambao anafahamiana nao akiwemo meneja wa Trey Songz, Kevin Riles na meneja wa Ludacris ambao licha ya kumuunganisha Platnumz kwa Kevin Liles ili amsaidie lakini pia aliwaomba waje Tanzania kusaidia wasanii wengine.


Ludacris na Chaka zulu


“Siku ya pili akaja kiongozi mwingine Chaka Zulu, Shakazulu huyu ndiye meneja wa Ludacris[…] amekuja Chaka zulu tumezungumza naye, na wote hawa hatimaye tumekubaliana kwamba watakuja[….] watakuja tarehe 11 July mpaka tarehe 23 July”. Alisema Rais Kikwete.

Aliendelea,
“Anakuja Terrence J, Terrence J huyu ndiye muasisi wa Black Entertainment Television, lakini sasa Terrence J ndiye anaendesha wale wanaoangalia kwenye televisheni Channel E! lakini Terrence J anakuja na mwanamuziki maarufu wa Marekani Usher, na bado hatujamaliza na Trey Songz anaweza kuja”. Alisema Rais Kikwete.
Previous Post Next Post