Video: T.I na The Game wakigombana na polisi baada ya washkaji zao kupigwa

Mwanahip hop  anayetokea Compton Marekani, The Game pamoja na rapper wa Atlanta ‘T.I’ walijikuta wakiingia katika mzozo na askari polisi kufuatia washkaji zao kuchezea kichapo toka kwa mabaunsa wa klabu moja ya usiku inayoitwa SuperbClub.


Ishu hiyo ilitokea baada ya kundi moja la watu waliodaiwa kufahamiana na mastaa hao kukataliwa katakata kuingia ndani ya ukumbi huo wa starehe. Baada ya mapolisi LAPD kuwasili eneo la tukio ndio walikutana na T.I aliyekuwa sambamba na The Game pamoja na wapambe wao marapa hao kuanza kuwalalamikia polisi hao kuhusika kwa namna moja au nyingine katika ugomvi huo

Tazama video za ugomvi wao hapa!




Previous Post Next Post