Picha: Diamond Platnumz akutana na Manager wa Trey Songz na Big Sean

Kweli baati ya mwenzio usiilalie mlango wazi , amini kuwa Diamond Platnumz halali. Pamoja na mafanikio makubwa anayoendelea kuyapata, staa huyo anazidi kujitengeneza connection kali za kimataifa.

Diamond akiwa na Kevin Liles, meneja wa Trey Songz, Big Sean, Estelle na wasanii wengine

Katika kile kinachoonekana kuwa ni mazungumzo ya mwanzo wa safari ya kuelekea kuanza kufanya collabo na wasanii wa Marekani, Diamond amekutana na meneja wa Trey Songz, Big Sean na wasanii wengine wakubwa, Kevin Liles.

Mmoja wa watu waliopo kwenye timu ya Diamond, Salam wa SK Entertainment, ameshare picha nay a Diamond akiwa na Kevin Liles na kuandika: “Don’t Ask Me Whats Next…. Please 2 Days to go… VOTE FOR @diamondplatnumz for MTV MAMA Awards BEST COLLABORATION AND BEST MALE.”
Previous Post Next Post