H.Baba aumwa ugonjwa wa Dengue, alazwa Muhimbili

Msanii wa muziki na filamu H.Baba amelazwa usiku wa kuamikia leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam baada ya kugundukika anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue.



H.Baba akiwa amelazwa hospital
Frora Mvungi ambae ni mke wa H.baba amesema:Dengue, Muhimbili now saa nane hii, usiku hali ilikuwa mbaya zaidi imebidi tuletwe Muhimbili Hospital.amegundulika ni dengue. thanx to god anaendelea vizuri and that is the last drip.asante my manager Yahya for your greatest help.mungu akuzidishie.asanteni pia my fans kwa maombi yenu.


H.Baba akipata dripi hapo jana kabla ya kuzidiwa na kukimbizwa Muhimbili
H.Baba alianza kujisikia vibaya jumatano (Juni 5) wakati anajiandaa kwenda kumuaga mtayarishaji wa filamu na vipindi vya TV , marehemu George Tyson aliyofariki wa ajali ya gari may 30.
Previous Post Next Post