Diamond Platnumz - Biography

Birth name : Naseeb Abdul Juma   Born  : 02 October 1989
Birthplace  :  Kigoma, Tanzania
Genres   :Bongo Flava
Years active  : 2009



Baada ya kuzaliwa 02/10/1989 Alfajiri mnamo wa saa kumi na moja katika Hospitali ya Amana jijini Dar-es-salaam /Tanzania Diamond alipewa jina la Nasibu Abdul Juma…Kutokana na tofauti kati ya mama na baba yake mwaka 1992 Nasibu na mama yake ilibidi wahamie Tandale Magharibi kwa bibi yake mzaa mama, na hapo ndipo yakawa makazi yao. Mnamo mwaka 1995 alianza kupata elimu ya Nursery katika shule ya Chakula Bora iliyopo Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu ya Msingi yaani (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi Tandale magharibi iliyopo jijin Dar-es-salaam. Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kucopy (cream) baadhi ya nyimbo za wasanii waliokuwa wakihit ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehem tofautitofauti. Mara nyingi mama ake alikuwa akimnunulia kanda za ulbum za wasanii tofauti waliokuwa wakihit kipindi hicho na hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, na wakati mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofautitofauti ya tallent show ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya kumuhimiza kimasomo. Kiukweli hali ya maisha yao ilikuwa ni ngumu saana, maana mama Diamond hakuwa hana source ya kumuingizia kipato, hivyo ilibidi atumie kias kidogo anachokipata toka kwa kodi ya vyumba viwili alivyopewa na Mama yake yaani bibi yake diamond na vibiashara vyake vidogovidogo vya mikopo kwa kumsomeshea na kumlea diamond, hakika hali yao ya Kimaisha ilikuwa ni ngumu sana, hivyo iliwaradhimu wote kuhamia katika chumba cha bibi huyo ili kupangisha vyumba vile viwili alivyopewa mama diamond… Baada ya kuhitimu shule ya Msingi mwaka 2002 na kutaka kuanza masomo ya Secondary mwaka 2003 mama yake alimwambia aachane na Muziki kabisa na azingatie na Masomo ili aweze kupata elimu itayomsaidia hata kwa muziki wake baadae kwa maana asingeweza kushika vitu viwili kwa pamoja muda huo. Akiwa secondary diamond aliendelea kufanya muziki kisirisiri bila mama yake kujua na kufikia mwaka 2004 taratibu akaanza kujifunza kuandika nyimbo zake mwenyewe. Baada ya kuhitimu elimu yake ya Secondary mwaka 2006 mwaka 2007 alijikita rasmi katkia sughuri za muziki ili kujaribu kutimiza ndoto zake.kiukweli haikuwa ni safari rahisi kama alivyotegemea hadi kupelekea time kuanza kutafta vibarua toafauti tofauti ili mradi aweze kupata rizki na kuepuka hali ya kushinda nyumbani, ikiwemo kuuza mitumba, petrol station, kupiga picha, kupigisha simu, kazi za viwandani hata wakati mwingine kuingia kwenye makundi ya kucheza kamali za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia studio kurecord lakini bila kufanikiwa, kiukweli ulikuwa ni wakati mgumu sana hadi ikamradhimu kuuza pete ya Dhahabu ambayo alipewa na mama yake mzazi aivae na kumdanganya kuwa ameipoteza na ndipo hapo alipofanikiwa kuingia studio kurecord nyimbo ya kwanza iitwayo tokamwanzo..kutokana na kutokuwa na mazoea ya kurecord hakuweza kutengeneza nyimbo ambayo ni hit lakini wimbo ule ulianza kumpa conections tofautitofauti maana wengi walishangazwa jinsi alivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kuweza kutengeneza wimbo kama mtu ambae ni mzoefu, hivyo iliwafanya kuamini kuwa akipata nafasi ya kurecord mara kadhaa angeweza kufanya kitu kikubwa.. wimbo ule ulimfanya aweze kukutana na Chizo mapene ambae alijitolea kumsimamia, na kweli wakaanza kurecord Ulbum lakini bahati mbaya wakiwa katikati ya uricordiji wa ulbum hiyo kijana huyo alipata matatizo ya kifedha na hakuweza tena kumsaidia hivyo ilimbidi  Diamond aanze tena upya, kuzunguka katika studio tofauti kuomba kusigniwa kwenye record label lakini kote hakuweza kufanikiwa, wote walimwambia bado kuimba hajui na kuto kutaka kumsikiliza kabisa…kiukweli kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana hata yule mpenzi wake ambae alikuwa nae alimuacha kwakua alikuwa ameshachoshwa na ndoto hewa ambazo alikuwa akiziota kila siku diamond kuwa ipo siku atafanikiwa kimuziki na kuwa mwanamuziki mkubwa na wao kuish maisha mazuri, kitu ambacho kilimchanganya na kumuumiza sana diamond hususan kwa kauli aliyomuambia ya “skiza Diamond mi kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana maslahi kwangu” kutwa ilikuwa ikimpitia kwenye kichwa na kujiona kama mwenye mikosi, mwaka 2009 diamond alikutana na Bwana Msafiri Peter almaarufu kama Papaa Misifa  na kukubali kumsaidia kimuziki na Kurecord wimbo wa kwanza ulioenda kwa jina la “Nenda kamwambie”, wimbo ambayo kuanzia A mpaka Z  Diamond kwa uchungu alimuimbia  mpenzi wake huyo aliyemuacha (Sarah Sadiki) kuelezea kias gani aliumia kwa yeye kumuacha kwake, na hapo ndipo taratiibu nyota yake ikaanza kung’aa na wimbo huo kukua (Kuvuma) siku hadi siku..Tareh 14/02/2010 Diamond alirelease ulbum yake ya kwanza iliokuwa na nyimbo 10 ambazo ni .1 kamwambie .2 Magala .3Nitarejea .4 Nalia na mengi .5 Binadamu .Nakupa .6 Usisahau .7 Uko tayari .8Wakunesanesa .9Toka mwanzo 10.Jisachi… 04/04/2010 Diamond aliandika record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tunzo tatu za Tanzania Kili Music Awards kwa pamoja ambazo ni: Msanii bora Chipukizi, Wimbo bora wa Mwaka (KAMWAMBIE) na Wimbo bora wa R&B(KAMWAMBIE), tunzo ambazo zilimfanya achaguliwe kuwa balozi wa Malaria nchini Tanzania….Baada ya kuachia wimbo wake wa pili (MBAGALA) Tarehe 31/08/2013 Diamond alichaguliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete kuwa Entertainer katika tour nzima ya Kampeni yake… Tareh 02/10/2010 alipata tour ya kwanza kwenda England mjini LONDON,MILTON KEYNES, na COVENTRY.. 02/12/2010 Diamond alichaguliwa kuwa Msanii bora Chipukizi katika tunzo za MTVBASE MAMAS AFRICA AWARDS zilizo fanyika nchini Nigeria… baada ya kurelease wimbo wake wa tatu mwaka 2011 Diamond alishinda tunzo ya Nzumari  Award nchini Kenya akiwa kama Msanii bora wa Kiume toka Tanzania… 02/10/2010 Diamond alirelease nyimbo yake ya nne na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza na pekee kujaza Club Maisha hadi watu kushindwa kuingia na hata wengine kuzimia baada kutokupata hewa ya kutosha kutokna na wingi ujaaji huo… 01/01/2012 alirelease Ulbum yake ya pili na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuuza zaidi ya 1200,000 ulbum Copies… Mwanzoni mwa mwaka 2012 diamond aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show ya Corparate kwa kiinglio cha shilingi elf hamsini 50,000 za kitanzania akiwa pekeake na show kuwa sold ot kwa zaidi ya ticket 1,500…8/04/2012 Damond alishinda  tunzo tatu za Kili Music Awards ikiwemo :1 Mtunzi bora wa kiume :2 Video bora ya Mwaka na :3 Mtumbwizaji bora wa Kiume… around may diamond aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza kufanya show na kujaza zaidi ya watu elf 10’000 kwa kiingilio cha 20,000 katika kiwanja cha Darlive huku akishuka na Helcopter kwenye Stage…mnamo june Diamond alifanya ziara yake ya Europe ikiwemo Italy, Holland, Sweden , Greece,  na kumalizia ziara yake ya arabuni nchini Masqat Oman….. mnamo Jully Diamond alisinda tunzo ya Nzumari Music Awards toka Kenya akiwa kama msanii bora wa kiume toka Tanzania… mwishoni mwa 2012 Diamond alienda kufanya ziara yake nchini America…. Baada ya kurelease nyimbo yake ya “Nataka kulewa” na “Kesho” mwezi wa kumi na mbili mwaka 2012 diamond alitajwa kuwa ni msanii wa kwanza anaelipwa Pesa nyingi kwenye Show toka Tanzania…. Mwanzoni mwa mwaka 2013 diamond alichaguliwa na Cocacola kuwa Brand Ambassador wa Kinywaji Cha Cocacola, na kufuatiwa na ziara yake ya esta Africa na ikiwemo Burundi Congo na Kenya n.k. na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza east Africa kuweza kupiga show pekeake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000… mnamo June 2013 Diamond alishinda tunzo mbili akiwa za Tanzania Kili Music Award akiwa kama :1 Msanii bora wa kiume Bongoflavour na :2 Msanii bora wa kiume kwa wanamziki wote Tanzania…  jully 2013 Diamond alirelease next single yake iliyokwenda kwa jina la Number One ambayo aliifanyia Video Capetown South Africa Chini ya kampuni ya Ogopa Videos.. na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza kulaunch video bila kiingilio katika Hotel ya SERENA na kuwaalika CEO’s MANAGER’s na viongozi toka sehem tofautitofauti ili waone kazi za vijana wao wa Tanzania zinavyoenda… na katika launching hiyo akamzawadia Gari moja ya Malegend wa kubwa katika mziki wa Tanzania mzee Mwidini Gurumo…. Mwezi wa 09/2013 diamond aliweka record ya kuwa Msanii wa kwanza toka Tanzania kusign mkataba wa kuuza ring caller direct na Kampuni ya VODACOM TANZANIA….mwezi 10/2013 diamond alifanya Collabo na msanii toka Nigeria Davido ya ngoma ya Number one kama Remix na kisha kwenda nchini Nigeria kwajili ya kusomea Markert ya West Africa na kushoot video ya wimbo huo ulio shootiwa na Kampuni ya Capital Dreams iliyo chini ya Director Clarence Peter ….
Previous Post Next Post