Sports Videos Music Radios Music Charts Tech Contact Us

Hitmaker wa nyimbo kama Salome,Julieta, Nyambizi na zingine nyingi, Dully Sykes ambaye wiki hii ametimiza miaka 15 tangu aingie kwenye muziki wa Bongo Fleva, amesema kuwa anatarajia kufungua studio na kuanza kufanya kazi za live na matangazo.


Dully akiwa studio
“Nafungua Studio kubwa kabisa kwa sababu ya live na matangazo,” aliiambia Clouds FM. “Sisemei kama hakuna studio bora zipo studio bora nyingi tu, kwahiyo itakuwa kati ya zile studio bora, sehemu ambayo naihamishia ni Bima Tabata. Wapenzi wa muziki wangu wanaopenda kufanya kazi na mimi nitaanza live sasa hivi, kwahiyo nitaanza kufanya na mabendi ili kutangaza biashara yangu,” aliongeza.

Previous Post Next Post