Shakira atoa video ya wimbo wake wa Kombe la dunia 2014 ‘La La La’ aliowashirikisha Messi, Pique, Neymar… Video: Shakira atoa video ya wimbo wake wa Kombe la dunia 2014 ‘La La La’ aliowashirikisha Messi, Pique, Neymar

Dili la wimbo rasmi wa kombe la FIFA la dunia kule nchini Brazil kwa mwaka huu lilimdondokea Pitbull na Jenniffer Lopez, ambao wamefanya wimbo uitwao ‘We Are One (Ole Ola), lakini mwimbaji wa Colombia Shakira ametoa video ya wimbo wake pia wa kusupport kombe hilo la dunia Brazil 2014 aliouita ‘La La La (Brazil 2014),’.



Shakira ambaye ndiye alifanya wimbo ramsi wa Kombe la dunia mwaka 2010 Afrika Kusini (Waka waka) uliopata umaarufu mkubwa , katika video ya wimbo mpya amewashirikisha mastaa wa soka akiwemo mpenzi wake na baba wa mwanaye Gerard Pique, Lionel Messi, Cesc Fabregas, Eric Abidal, Neymar, James Rodríguez, Sergio Agüero, na Radamel Falcao. Pia mwanaye aitwaye Milan anaonekana kwenye video hiyo.

Mashabiki wengi wamejaribu kuzishindanisha nyimbo hizi mbili kati ya huu mpya wa Shakira na wimbo rasmi wa mwaka huu wa Pitbull na J.LO.



X


wewe unahisi upi unavuta zaidi kwa mashindano ya mwaka huu?
Huu ndio wimbo rasmi wa Pitbull na Jennifer Lopez

Previous Post Next Post