Nisha: Naona aibu kuangalia filamu zangu za komedi

Yule msanii wa sanaa za vichekesho nchini, Salma Jabu aka Nisha amesema huingia na aibu kutazama filamu zake za komedi kutokana na vituko anavyovifanya.

Nisha akiwa katika picha ya utengenezaji wa filamu yake mpya ya Zena na Betina



Hapa Nisha akiwa katika anahigiza katika scene yake ya movie ya zena na Betina
Nisha anayetamba na filamu kama Pusi na Paku,Tikisa,Gumzo na Zena na Betina amedai anapoangalia filamu zake halafu mtu akamkumbushia hujificha uso wake kwa aibu.


Nisha akitoa hisia zake kwa shabiki aliyekuwa akimsifia kwa kazi zake
“Ni ngumu kuamini but huo ndio ukweli, hata mimi nikijitazama huwa naona aibu,ndugu zangu hawaamini yule mtoto mpole anayeng’ata kidole hadi ukubwani,Leo kwenye tv anafanya hayo.. Thanx God ujumbe umefika nimeweza kuwafanya watu waamini mimi mcharuko hahaah,” amesema Nisha.
Previous Post Next Post

Popular Items