Nay wa Mitego aongea kuhusu kusambaa kwa picha ya mchumba wake akivishwa pete na ‘pedeshee’

Hatimaye Nay wa Mitego amezungumzia scandal iliyokuwa ikimhusu mchumba wake aitwaye Siwema ambaye mwezi uliopita ilisambaa video na picha kwenye mtandao wa Instagram inayomuonesha akivishwa pete na pedeshee.



Siwema akiwa na pedeshee kwenye sherehe ya kuvishana pete
Maelezo kuhusu video/picha hizi yalisema:

“Siwema demu wa Nay Wa Mitego amevalishwa pete ya uchumba na jibaba ( pedeshee ) linalomuweka mjini na ndilo lililomnunulia magari mwanzo aina ya Verosa na baadaye Kluger halafu Verosa akampa Nay wa Mitego, sasa hivi kamnunulia Lexus harrier… Inasemekana Nay pia analelewa na huyo dingi maana amekubalije amegewe demu na kuhongwa gari alilohongwa demu wake.”


Ney akiwa na Siwema 

Pia kupitia mtandao huo, picha za msichana huyo zinazomuonesha akiwa nusu utupu zilisambaa.

Akiongea kwenye kipindi cha So So Fresh cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay alisema ni kweli Siwema alimkosea lakini amemsamehe.


Mimi Siwema ni mwanamke ambaye nampenda kila mtu anafahamu maybe ndio maana ilikuja kuwa tatizo. Kuna vitu vilitokea mimi nilikuwa sifahamu kama nilivyosema kuna watu wakanifuata wenye nia zao sielewi mtu alikuwa na nia gani wakiviweka Instagram na kwenye mtandao. Mimi mwanamke wangu najua alinikosea. Sikujua kilichokuwa kinaendelea lakini hakuweka wazi. Ni kitu ambacho kilitokea kabla ya mimi kuwa naye lakini hakuwahi kuniambia kwamba kilitokea mpaka wakafikia hatua ya design hiyo, hilo ni kosa ambalo alinikosea. Tuliyamaliza, mimi ni gangster ambaye na nina mwanamke ambaye nampenda. Huwezi kumwacha mwanamke kwasababu ya kitu ambacho ni cha historia, sidhani kama ni fair. Pia ni mwanamke ambaye mimi nipo naye kwasababu tunapendana halafu ni mwanamke ambaye ananielewa na tunaelewana na ndio maana niliamua kumweka wazi kila mtu anamfahamu. Hata kama itakuwa vyovyote vile, siwezi kumwacha hata siku moja. Kweli ni kosa kubwa ambalo linahitaji moyo kwaajili ya kumsamehe mtu lakini naamini nimefunzwa kusamehe kwenye mahusiano, hili ni la kwanza acha lipite mwenyezi Mungu atusaidie tuendelee kudumu. Mimi nipo bado na Wema na maisha yanaendelea.”
Previous Post Next Post