Video: Tyrese aungana na Dr. Dre kusherehekea ubilionea wake 'Billionaire boys Club'

Inaonekana wazi kuwa Dr Dre ameshaafikiana na Apple kuhusu kuwauzia kampuni yake inayotengeneza headphones kwa $billion 3.2.

Mtayarishaji huyo wa muziki ameonekana katika video akisherehekea kuwa billionaire wa kwanza mwana hip hop huku akipewa shavu na muigizaji wa First and Furious, Tyrese Gibson.



Katika video hiyo, Tyrese anaonekana akishangilia na kuwataka Forbes warekebishe mapema orodha ya wanahi hop matajiri zaidi duniani, “the Forbes list just changed..”

Nae Dr Dre alionekana akitamba kuwa billionaire wa kiwanza tena kutoka West Coast, “The first billionaire in hip hop, right here from the motherf***ing West Coast!”



Kama mpunga huo ($billion 3.2) utaingia kwenye akaunti ya Dr Dre ambaye anatarajia kupata share ya zaidi ya $ billion 1 atakuwa amemzidi karibu mara tatu P.Diddy ambaye anaongoza orodha ya wana hip hop matajiri zaidi duniani kwa kuwa na utajiri wa $million 700, akifuatiwa na Dr. Dre mwenye $million 500.
Previous Post Next Post