Hawa Ndio wanawake100 wenye nguvu Dunaini kwa mwaka 2014, Beyonce, Shakira, Lady Gaga waingia kwenye orodha ya mwaka huu 'Forbes'

Jarida Maarufu Duniani la Forbes Jumatano hii limetoa orodha mpya ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani (100 Most Powerful Women ) 2014, ambayo imeongozwa na chancellor Angela Merkel wa Ujerumani.



Beyonce ni miongoni mwa wanawake walioingia katika orodha hiyo ya Forbes akiwa ameshika nafasi ya 17. Wanawake wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Hillary Clinton katika nafasi ya 6, Michelle Obama no.8 na Oprah Winfrey amekamata no 14.


Wanawake wengine maarufu waliotajwa ni Angelina Jolie kwenye nafasi ya 50, Mcolombia mwimbaji Shakira katika nafasi ya 58, Lady Gaga amekamata nafasi ya 67.




Previous Post Next Post