Studio ya Quick Racka ‘Switch Records’ yapata Producer mpya na rasmi, ni Nahreal

Quick Rocka ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania wanomiliki studio zao, lakini toka studio yake imefunguliwa alikuwa bado hajaweka wazi producer atakayekuwa mpishi wa studio hiyo inayoitwa ‘Switch Records’.



Quick amemtangaza rasmi Nahreel ndiye producer wa Switch.

‘It’s official now…He’s the producer at SWITCH REC. @NahreelBeatz #2014#Switch#Midundo#MoneyTeam#Nahreel’ ameandika Quick kupita Instagram.

Nahreel ni producer ambaye amefanya hits nyngi hadi sasa zikiwemo kazi nyingi za Weusi, single ya Vanessa ‘Come Over’ na wimbo wa kundi lake Navy Kenzo ‘Chelewa’.



Wasanii wengine wanaomiliki studio zao ni pamoja na Professor Jay, Dullysykes, Bob Junior, Mrisho Mpoto, Mb Dogg, Juma Nature, AT na wengine.
Previous Post Next Post