Real Madrid yaifunga Bayern Munich

Real Madrid imeibuka kifua mbele katika mechi ya kwanza ya nusu ya fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich.

Mchezo huo umechezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabéu, Madrid huku bao hilo pekee likiwekwa kimiani na mshambuliaji Karim Benzema dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza!

Karim Benzema (kushoto) akiifungia Real Madrid bao pekee. Kulia ni mchezaji wa Bayern Munich, David Alaba.
Wachezaji wa Madrid, Pepe (kushoto) na Sergio Ramos (katikati) wakiondosha hatari langoni mwao.
Cristiano Ronaldo (katikati) akiwania mpira na Alaba (wa pili kushoto) na Dante.

Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA