Muigizaji wa filamu ya maisha ya Mandela Idris Elba apata mtoto wa kiume

Muigizaji maarufu duniani na raia wa Uingereza, Idris Elba na mpenzi wake Naiyana Garth wamepata mtoto wa kiume Alhamisi ya wiki hii.



Idris Elba ambaye ameigiza filamu inayoelezea maisha ya Mandela na harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini inayoitwa ‘Mandela: Long Walk To Freedom’ alishare picha za mtoto wao kwenye twitter Ijumaa na kulitaja jina la mtoto wake.
“My son, Winston Elba, was born yesterday. Truly amazing.” Alitweet.

Huyo anakuwa mtoto wa pili kwa muigizaji huyo ambaye ni mshindi wa tuzo za Golden Globe kwa kuwa tayari ana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliyezaa na mkewe wa zamani, Dormowa Sherma
Previous Post Next Post

Popular Items