Kaka zake Paul Walker kuchukua nafasi yake kwenye Fast and Furious 7

Waandaji wa Fast and Furious 7 wameeleza kuwa nafasi ya marehemu Paul Walker katika filamu hiyo itachukuliwa na kaka zake Celeb na Cody.

Pichani:Paul Walker na ndugu yake

Paul Walker alikuwa akiigiza kama Brian O’Conner katika mfululizo wa Fast and Furious akiwa na timu ya mastaa wenzake kama Tyrese, Vin Diesel na Ludacris.

Katika tamko lao waliloweka kwenye ukurasa wao wa Facebook, waandaaji hao wameeleza kuwa filamu hiyo itakamilika na kutoka mwaka 2015.

Paul Walker alifariki kwa ajali ya gari November mwaka jana.
Previous Post Next Post

Popular Items