Exclusive: Rich Mavoko kufanya show nane katika nchi za Ulaya, ni kwa mara ya kwanza

Bongo Flava inalipa na inazidi kuwatoa wasanii wengi nje ya mipaka ya Tanzania ambapo tumewasikia baadhi ya wasanii wakubwa wakipata shows nje ya nchi.

Mwimbaji wa Roho Yangu, Rich Mavoko ana kila sababu ya kufurahia matunda yanayoendelea kuongezeka katika shina la muziki mzuri anaoufanya ambapo hivi karibuni ataingia barani Ulaya kufanya shows zisizopungua nane ikiwa ni kwa mara ya kwanza anafanya show nje ya bara hili.



“Mungu akijalia naweza nikaenda Europe na naenda kufanya shows kama nane hivi. Kwa hiyo my manager ndio alikuwa anahangaikia hivyo vitu…vitu vyote hivyo yeye ndiye anafanya. Kwa hiyo Mungu awabariki, nijaribu kutoka.” Rich Mavoko ameiambia tovuti ya Time Fm.

Rich Mavoko ameeleza kuwa ziara hiyo ni matunda ya wimbo wake wa Roho Yangu ambao umempa shows nyingi zaidi ndani ya nchi na sasa ameanza kutoka nje ya nchi, na kwamba ni wimbo mkubwa ambao yeye pia anauheshimu sana.

Hata hivyo, mwimbaji huyo amesema bado ni mapema kutaja nchi na tarehe rasmi atakayoondoka lakini ameshacomfirm na anasubiri kukamilisha taratibu nyingine.

“Kuna vitu naviweka sawa. Kwa hiyo vikishakuwa sawa nitatangaza naenda wapi na wapi. Lakini vitu viko tayari yaani.”

Rich Mavoko anakuwa msanii wa pili kuelekea Ulaya hivi karibuni. Ben Pol yeye atafanya show Munich, Ujerumani April 30 mwaka huu.
Previous Post Next Post