Ice Prince asema bado ajafikiria kabisa suala la kuoa

Rapper kutoka Nigeria Ice Prince ataendelea kula ujana kwa kuwa suala la kuoa bado halijamuingia kichwani kwa hivi sasa.

Rapper Ice Prince


Rapper huyo amesema kuwa licha ya kuwa ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 2 hafikirii kumuoa mama wa mtoto wake aitwae Bimbo Babatunde wala mrembo yeyote kwa hivi sasa kwa kuwa yeye anajiona bado ni kijana mdogo.

“I don’t think I am planning to get married now because am still young, I’m in my youth and moreover, I am just 27 years old. Maybe later in my late thirties I can start planning to get married or not.” Ice Prince ameliambia jarida la Vanguard la Nigeria.

Ameongeza kuwa bado ana safari ndefu hadi kufikia kuamua kutulia na kuoa, hivyo anaitaji kujifunza na kuelewa kabla ya kuamua.
Previous Post Next Post