Ukisikia unaambiwa mwaka huu ni wa Diamond usikatae 'Hapa nikiwa na maana ya kwamba bahati/kismatichake kinazidi kupanuka siku hadi siku' Na sasa muimbaji wa kike anayeaminika kuwa maarufu na mwenye kipaji zaidi nchini Nigeria, Waje amemzungumzia staa huyo wa Tanzania kuwa ni mtu mnyenyekevu mwenye nidhamu kubwa ya kazi.
Met this amazing brother yesterday, humble nd such an inspiration,his work ethic is super. #africanlegendsmakingmusic @diamondplatnumz the talent eh. Thanks so much for this honour,” ameandika Waje kwenye Instagram.
Unaweza usiwe unamfahamu vizuri Aituaje Iruobe maarufu kama Waje lakini hakuna ubishi kuwa umewahi kusikia sauti yake. Waje ndiye msichana anayesikika kwenye hit single ya P-Square ya mwaka 2008, Do Me. Na sasa muimbaji huyo atasikika kwenye wimbo aliomshirikisha Diamond Platnumz.
DJ Fetty wa Clouds FM aliyeongozana na muimbaji huyo wa ‘My Number One’ aliandika. “In the booth right now. Its @diamondplatnumz featured in @officialwaje coming ish in Nigeria and Africa at large,” ameandika Fetty kwenye kipande cha video alichokiweka kwenye Instagram.
Katika hatua nyingine, Diamond amewataka vijana wa Tanzania kujitikita zaidi kwenye kilimo na kupotezea ile imani kuwa kilimo ni ushamba.

“Unajua tusichukulie kama suala la kilimo kwamba mtu ukilima unakuwa mshamba,” staa huyo alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM jana. “Unakuwa mtu wa zamani,kwa sababu unaweza kuwa na swagga zako na unalima, cha muhimu ni kuangalia un invest vipi katika kilimo, katika sector zipi,kuna sector nyingi sana za kuwekeza katika kilimo. Kwasababu ukiangalia nguo tunazovaa,chakula tunachokula, vyote vinatokana na kilimo, so ukiweza kujua nitumie fursa gani kwenye kilimo unaweza kupata pesa nyingi sana. Ukiangalia hata tajiri wa kwanza Afrika anatokana na kilimo ‘Dangote’ so unaweza kuajiri watu kama umebahatika kuwa nanihii,kwasababu sisi waswahili wengi sehemu tunazoishi sisi tunaweza hata kuweka vimatembele vinini,yani vitu vitu fulani ambavyo vinaweza vikakusaidia. Na kwa wale wenye kubahatika wana mashamba tunaweza tukawaweka watu, kwamba sisi tunakaa town kuuza sura,tukawaweka watu ambao wanatulimia, cha umuhimu ni kufikiria unalima kitu gani ambacho kitakuingizia,sio ulime tu mradi unalima lakini kitu ambacho kitakuingiza hela kipo. Watu lazima wale. Tofautisha ukiuza nguo kuna watu wanaweza wasinunue akavaa nguo ya jana,lakini mtu hawezi sema nishakula jana leo sili lazima ale.”