Hizi ndizo trend za fashion zilizowateka celebz hawa hapa Bongo 2014.

Mtindo maarufu ujulikanao kama Way:
ukiangalia kuanzia juu mpaka chini unaweza kuona kila celeb anajitahidi kutoka kitofauti ila hapa kwenye haircut ni moja kati ya style ambayo inaonekana kuwateka wasanii wengi tu maarufu hapa bongo,kuanzia shetta,jux na ommy dimpoz etc, na kufanikiwa kurudisha style ya way tena kwa mara nyingine back katika fashion trend ya 2014.


Sunglasses hizi:Kama unakumbuka nyimbo za msanii shagy za zamani,ndio utashtukia mchezo mzima kuwa vitu vya zamani ikiwemo hii aina ya miwani ya jua ndio iliyokuwa inatesa sana kipindi hicho na kwa 2014 ndio imerudi na kuwa ndio trend ya fashion ambayo imefanikiwa kuwateka celeb wengi sana duniani,na hata hapa kwetu nyumbani.

Red sneakers:Katika upande mwingine wa mtoko wa viatu unaweza kusema kuwa siku za valentine zinaendelea cause ,imekuwa fashion nayo kwa mwaka huu kwa viatu vyekundu kuvaliwa kwa sana na celebrities wengi wa hapa bongo zaidi kuliko miaka yote iliyowahi kutokea,unaweza kusema ndio rangi ya viatu inayotamba kwa mwaka huu but its too early to say cause mwaka ndio kwanza unaanza ila inaonekana kuwa ndio mpango mzima kwenye upande wa rangi ya raba.

Previous Post Next Post